Kitu Afande Sele kaongea toka ajivua uanachama ACT-Wazalendo….



 
Ni msanii mkongwe Afande Sele kutoka Tanzania alitangaza kujivua  uanachama wa ACT Wazalendo.Kilichomfanya Afande Sele a-trend kwenye mitandao ya kijamii Dec 15 2016 ni baada ya kuchukua maamuzi hayo ya kujiondoa ndani ya chama hicho cha ACT- Wazalendo.

Baada ya hapo wengi wametoa maoni yao kwenye mitandao ya kijamii kuhusu maamuzi ya Afande Sele na usidhani kwamba Afande Sele  mwenyewe hajayasoma, sasa kupitia kwenye Exclusive na Ayo TV na millardayo.com amesema>>>> Ni kweli Dec 15, 2016 nimetangaza rasmi kujiondoa ACT- Wazalendo yaani kujitoa katika masuala ya siasa na sipo katika chama chochote cha siasa sasa hivi mimi ni mtu huru’


    ‘Nimejitoa ACT- Wazalendo kwa makusudi kabisa na hili lilikuwa ni jambo tarajiwa, kitu cha kwanza moja ya matarajio yalikuwa baada ya mimi kuingia ACT nakuwa Mbunge ila sasa sikupata Ubunge na kama ningeupata Ubunge basi nisingejitoa ndani ya chama’
Kitu Afande Sele kaongea toka ajivua uanachama ACT-Wazalendo….  Kitu Afande Sele kaongea toka ajivua uanachama ACT-Wazalendo…. Reviewed by Unknown on 5:47 AM Rating: 5

No comments