Polisi Waua Wawili kwa Tuhuma za Ujambazi

Polisi wilayani Rungwe wamewaua watu wawili kwa tuhuma za ujambazi baada ya kuanza kufyatua risasi kwa polisi waliokuwa wakiwafuatilia.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Dhahiri Kidavashari amesema leo kuwa tukio hilo limetokea katika Tarafa ya Pakati wilayani humo baada ya polisi kuwafuatilia watu waliokuwa na nia ya kwenda kufanya ujambazi katika duka la mfanyabiashara wa soda na bia za jumla na M-Pesa katika Kijiji cha Kisiba.
Alisema majambazi watatu walipakizana kwenye pikipiki moja na baada ya kuwaona polisi walianza kufyatua risasi na hatimaye polisi walijibu na kuwajeruhi wawili kati ya watatu huku mmoja akifanikiwa kutimua mbio baada ya kuitupa bunduki.
Polisi Waua Wawili kwa Tuhuma za Ujambazi
Reviewed by Unknown
on
10:54 AM
Rating:

Post a Comment