Yusuf Manji Mahakamani Tena Kesho

Kesi inayomhusu Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ya juu ya
matumizi ya dawa za kulevya aina ya Heroine, inatarajiwa kusikilizwa tena kesho
Alhamisi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya kuahirishwa kwa mara
ya mwisho Februari 16, mwaka huu.
Manji anatuhumiwa kutumia madawa hayo kinyume na sheria ya mwaka
2015 ya kuzuia na kupambana na madawa ya kulevya kifungu cha 17 (1) namba 5
ambapo inadaiwa Manji alitumia dawa hizo Februari 6 na 9, mwaka huu.
Kesi hiyo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian
Mkeha huku upande wa Jamhuri ukiwakilishwa na Wakili Osward Tibaloyekomya huku
upande wa Manji ukiongozwa na Wakili Alex Mgongolwa.
Baada ya kusikilizwa kwa mara ya kwanza kwa kesi hiyo, Manji
alikataa mashtaka hayo na kuachiwa nje kwa dhamana ya milioni 10 iliyotolewa na
Katibu wa Yanga, Charles Mkwasa.
Lakini kuna uwezekano mkubwa wa kusikilizwa kwa kesi hiyo
bila ya Manji kuwepo kutokana na kuumwa kwani kwa sasa amelazwa kwenye
Hospitali ya Aga Khan ambapo anasumbuliwa na tatizo la moyo
Yusuf Manji Mahakamani Tena Kesho
Reviewed by Unknown
on
6:52 AM
Rating:

Post a Comment